AFISA ELIMU SEKONDARI NDANI YA FOUNTAIN GATE DODOMA

AFISA ELIMU SEKONDARI NDANI YA FOUNTAIN GATE DODOMA.

Shule yetu @fountaingatesecondary imetembelewa na Afisa Elimu Sekondari Jiji la Dodoma Bi. Upendo Rweyemamu kwa lengo la kuzungumza na wanafunzi wa kidato cha pili pamoja na kidato cha nne ambao wanakabiliwa na mitihani ya kitaifa siku chache zijazo.

Mazungumzo hayo yamelenga kuwajenga wanafunzi katika kujiamini wanapofanya mitihani yao, kufuata taratibu za mitihani lakini pia kuendeleza matokeo bora katika jiji la Dodoma ambapo kwa miaka ya hivi karibuni wastani wa ufaulu umeongezeka.

Hata hivyo, watahiniwa wa kidato cha pili pamoja na kidato cha nne wamemuahidi Bi. Rweyemamu kuwa wamejipanga vyema na watafanya vizuri katika mitihani hiyo inayowakabili.

Aidha, akizungumza na @fga_tv mara baada ya kuzungumza na watahiniwa, Bi. Rweyemamu ameonyesha kufurahishwa na mazingira ya Shule ya Sekondari Fountain Gate huku akisisitiza kuwa @fountaingatesecondary inayo mazingira mazuri na tulivu kwa wanafunzi kujifunza na kupata elimu stahiki kwa ufaulu bora zaidi.

#YesWeAreFountain

Fountain Gate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts